Pages

Ads 468x60px

Featured Posts

Wednesday, May 30, 2012

UMEKUCHA UCHAGUZI YANGA SC

 Katibu wa kamati ya uchaguzi ya Yanga Francis Kaswahili (pichani) akizungumzia uchaguzi huo ambapo amewataka wanachama wote ambao hawajalipa ada kufanya hivyo ili kuweza kushiriki katika mkutano huo. 
Alisema kupitia uchaguzi huo zitajazwa nafasi za Mwenyekiti,Makamu Mwenyekiti na wajumbe wanne ambapo wanachama wayakaowania uongozi wanatakiwa kuwasilisha fomu zao wakiambatanisha risiti ya kununulia fomu, vyeti vya shule, uthibitisho wa uraia, namba ya uanachama na picha mbili za passport size.

STARS WAKABIDHIWA BENDERA, KUWAFUATA KINA DROGBA KESHO

 NAibu waziri wa habari, vijana, Utamaduni na Michezo Amos makalla akimkabidhi bendera ya Taifa Nahodha wa Stars Juma Kaseja, wakati wa hafka ya kuiaga timu hiyo leo kwenye hoteli ya Tansoma.Stars inaondoka alfajir ya kesho kwenda Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wao wa mchujo wa komve la Dunia utakaopigwa juni mbil.Wengine ni meneja wa bia ya Kilimanjaro inayoidhamini9 timu hiyo George Kavise, Mwenyekiti wa BMT Dioniz Malinzi na Kocha wa Stars, Kim Poulsen.
 Nahodha wa Stars Juma Kasejha akizungumza machache
                                                    Baadhi ya wachezaji wa Stars
                                                  Baadhi ya wachezaji waliohudhuria hafla hiyo leo

KOCHA STARS AWAASA NYOTA WAKE KUTOWAHOFIA KINA DROGBAA DROGBA


KOCHA mkuu wa timu ya Taifa Taifa Stars amewataka wachezaji wake kutohofia nyota waliopo katika kikosi cha  Ivory Coast  kwani hawana tofouti na wao.
Stars na Ivory Coast watkawaana  Juni 2, mjini Abidjan, katika mechi ya kuwania kucheza fainali za kombe la
dunia ambapo kikosi cha Ivory Coast kinawachezaji wanaosakata soka la kulipwa barani Ulaya wakiwemo  Didier Drogba, . Yaya Toure na Solomon Kalou na wengineo.
Kim alisema wanaiheshimu Ivory Coast kama moja ya timu yenye wachezaji wazuri lakini hawaihofii kwani wachezaji wa Stars pia ni wazuri ingawa wanatofaitiana vitu vidogo vidogo tu.
Kocha huyo aliwataka wachezaji wake kupambana kadiri wawezavyo katika mchezo huo kwani  ndio siri ya ushindi na mafanikio ya timu yoyote.

NYOSO,UHURU SELEMAN WAITESA YANGA


 KLABU ya Yanga imeanza mkakati wa kuwasajili wachezaji kadhaa kutoka kwa watani wao Simba, wakiwamo mabeki Juma Jabu, Juma Nyoso na kiungo Uhuru Suleiman.
Kwa mujibu wa habari zilizoifikia Tanzania Daima na kuthibitishwa na mmoja wa viongozi wa klabu hiyo anayehusika na usajili, wameamua kuwafukuzia nyota hao kutokana na mikataba yao Simba kukaribia mwishoni.
Chanzo hicho kimedokeza kuwa, kwa sasa wapo kwenye mazungumzo ya awali na nyota hao, ingawa bado hawajafikia hatua ya mwisho kwa ajili ya kusaini fomu za usajili kwa msimu ujao wa Ligi Kuu.  

Yanga imekuwa na mkakati wa kusuka kikosi cha ushindi baada ya kushindwa kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu iliyofikia tamati Mei 6, ikimaliza nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam FC.
Kama unavyojua, Yanga imekuwa mbovu katika siku za hivi karibuni na matokeo yake tulipoteza ubingwa wa  Ligi Kuu Bara na nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa msimu ujao, sasa hatutaki kurudia makosa, tunataka kufanya usajili mzuri kurejesha heshima yetu,” alisema kiongozi huyo.
Aliongeza, mbali ya hao,  pia wana mpango wa kuimarisha safu ya ushambuliaji kwa kusajili wawili kutoka nchini Rwanda ambao ni Meddie Kegere na Olivier Karekezi, waliong’ara kwenye michuano ya Kombe la Chalenji, lililofanyika Desemba, 2011, jijini Dar es Salaam.
Chini ya ufadhili wa Yusuf Manji aliyerejea kuokoa jahazi, Yanga wamepania kusajili nyota mahiri na kuajiri kocha bora atakayeziba nafasi ya Mserbia, Kostadin Papic, aliyemaliza mkataba wake mapema mwezi huu.

MISS DAR INTER COLLEGE YAZIDI KUSHIKA KASI

 Baadhi ya warembo wanaowania taji la Miss Dar Inter College 2012 wakiwa katika pozi mara baada ya mazoezi yao ya kila siku yanayofanyika kwenye hoteli ya Lamada jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa warembo hao Marylydia Boniface akiwapa maneno mawili matatu warembo hao.

VIONGOZI WAPYA RT WAANZA MIKAKATI

 BAADHI ya viongozi wapya wa chama cha Riadha Tanzania (RT) wakijadiliana masuala mbalimbali kuhusiana na chama hicho mara baada ya kuchaguliwa hivi karibuni.
Kutoka kushoto ni Tullo Chambo (Mjumbe) Suleiman Is-haq (Mweka Hazina) na Suleiman Nyambui (Katibu Mkuu) pamoja na mdau wa mamapipiro blog, Maria Kayala.


STAMINA TATIZO LA WACHEZAJI TANZANIA-POILSEN



WAKATI kikosi cha timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, kikitarajia kuondoka alfajiri ya kesho kwenda Ivory Coast kwa mechi ya kimataifa, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kim Poulsen, amesema stamina ni tatizo kubwa kwa nyota wengi.
Poulsen aliyetwaa jukumu hilo hivi karibuni kutoka kwa Jan Poulsen, aliyasema hayo jana wakati akitoa tathmini fupi juu ya mazingira ya kikosi chake tangu akabidhiwe jukumu hilo wiki mbili zilizopita.
Alisema, pamoja na wachezaji wengi kuwa na uwezo mkubwa kiuchezaji, suala la stamina limekuwa tatizo kwa wachezaji wengi, hivyo kushindwa kucheza kwa kasi na ufanisi kwa dakika zote 90.
Alisema kutokana na dosari hiyo, tayari ameanza kuchukua hatua kwa kufanya mazungumza na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuangalia njia bora ya kuondoa tatizo hilo kwa kushirikiana na makocha wa timu nyingine.
“Kwa upande wa Stars, nimeshaanza nalo kwa kuwapa  mazoezi ya ziada baada ya mazoezi ya kawaida. Kwa kweli, wachezaji wameonekana kuyakubali,  wameridhishwa nayo na kuyafurahia, binafsi inanitia moyo,” alisema.
Kim alisema mbali ya stamina, pia amekuwa akiwasihi wachezaji wake kuwa na moyo wa kujituma, akisema hicho ni kitu muhimu kwa timu katika kupigania ushindi na mafanikio ya timu.
Aidha, Poulsen alisema ndani ya kipindi cha wiki mbili alizodumu na timu hiyo, wachezaji wameanza kuelewa falsafa yake, hivyo kumpa matumaini ya kuwa na kikosi bora zaidi katika siku za usoni.
Hata hivyo, ameishauri TFF kuwa, wachezaji wote ambao watakuwepo kambini kipindi cha maandalizi ya mechi, wote wawe wanasafiri na timu (hata kama hawatacheza), kwa lengo la kuwapa nafasi ya kujifunza zaidi.
Katika hatua nyingine, Kim amekana kufanya upendeleo katika uteuzi wa kikosi cha kwanza, hasa katika mechi ya kirafiki dhidi ya Malawi, akisema alichagua kutokana na uwezo na sifa zao.
Aliongeza kuwa, nyota wake Nurdin Bakari na Thomas Ulimwengu  watabaki kutokana na kuwa majeruhi waliyopata wakati wa mazoezi yao, hivyo watabaki kujinoa kabla ya kuungana na wenzao watakaporudi kujiandaa dhidi ya Gambia.
Nyota wa Stars ni makipa: Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar). Mabeki: Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba).
Viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba - U20), Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20).
Washambuliaji ni Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Ramadhan Singano (Simba -U20), Simon Msuva (Moro United - U20),  Haruna Moshi (Simba) na John Bocco (Azam). 

15 WAJITOSA MISS KIGAMBONI CITY 2012

Na Mwandishi Wetu
JUMLA ya warembo 15 wamejitokeza kushiriki katika shindano la  kumsaka malkia wa kitongoji cha Kigamboni mwaka huu 'Miss Kigamboni City 2012' ambalo litafanyika Juni 15 kwenye ukumbi wa Navy Beach ulioko huko Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng'itu  (pichani) alisema kuwa maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri na bado milango iko wazi kwa warembo wengine wanaotaka kuwania taji hilo ili kutoa nafasi ya kupata mwakilishi atakayefanya vyema kwenye ngazi ya kanda na taifa hapo baadaye.
"Bado hatujafunga milango, tunawakaribisha wasichana wenye sifa kujiunga ili tuweze kupata mshindi atakayepeperusha kitongoji cha Kigamboni vizuri," alisema mratibu huyo.
Alisema kuwa kampuni yake ya K & L iliyopata baraka za kuandaa shindano hilo imejipanga kuhakikisha shindano la mwaka huu linakuwa bora na kuwapata washiriki watakaokwenda kutwaa taji la Kanda ya Temeke na hatimaye taji la taifa la Redd's Miss Tanzania baadaye mwaka huu.
Aliwataja warembo ambao wameshaanza mazoezi chini ya Hawa Ismail ambaye alikuwa Miss Temeke mwaka 2003 kuwa ni pamoja na Caroline Peter, Theopisther Wenso, Sophia Martime, Amina Aboubakar, Aisha Rajab, Rosemary Peter, Mariam Mbulilo, Julieth Phili, Doreen Kweka, Agness Goodluck, Khadija Kombo, Lina David, Aisha Mussa, Edda Silyvester, Fatina Francis na Rosemary Deogratius.
Alisema kwamba shindano hilo linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's, Dodoma Wine, Screen Masters, Clouds FM, Times FM na NSSF.
Taji la taifa la shindano hilo linashikiliwa na Salha Israel ambaye alitokea katika Kanda ya Ilala.

Tuesday, May 29, 2012

ANGETILE OSIAH ANG'ATUKA YANGA SC


KATIBU mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Angetile Osiah ametangaza kujivua nafasi yake ya ujumbe wa kamati ya uchaguzi ya klabu ya soka ya Yanga.
 Osiah amesema kuwa  analazimika kufanya hivyo kwa mujibu wa kanuni za uchaguzi za shirikisho hilo na atawasilisha barua kwa katibu mkuu wa Yanga, Mwesiga Selestine. 
Alisema kuwa licha ya kuteuliwa muda mrefu kushika wadhifa wa ukatibu wa TFF, alishindwa kuwasilisha barua ya kujitoa katika kamati ya uchaguzi kutokana na kuingwa na majukumu ndani ya shirikisho hilo
“Nimelazimika kufanya hivyo kwani kwa sasa Yanga inahitaji kufanya uchaguzi mdogo kwa lengo la kuziba nafasi zilizoachwa wazi na baadhi ya viongozi walioachia ngazi Yanga hivyo inabidi nafasi yangu ijazwe ili kamati iweze kuendesha mchakato wake kikamilifu,”alisema. 
TFF kupitia kamati ya uchahizi iliyo chini ya mwenyekiti wake Deogratius Lyato iliiagiza kamati ya uchaguzi ya Yanga chini ya mwenyekiti wake Jaji John Mkwawa ifanye uchaguzi wake kuziba nafasi za nane za viongozi waliojiuzulu na mjumbe mmoja aliyefariki dunia. 
Hatua hiyo inafuati hivi karibuni kujiuzulu kwa mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga kutokana na shinikizo la baadhi ya wanachama wakiongozwa na baraza la Wazee waliomtaka kufanya hivyo kwa madai ya kutoiletea mafanikio klabu na hatimaye kupokwa ubingwa wao wa ligi kuu bara ulioenda kwa Simba na wao kuishia nafasi ya tatu. 
Awali makamu mwenyekiti wa Yanga Davis Mosha alitangaza kujiengua katika uongozi miezi michache baada ya kuchaguliwa kwa madai ya kutoelewana na Nchunga, huku mjumbe wa kamati ya utendaji, Theonest Rutashoborwa alifariki dunia. 
Kama hiyo haitoshi, wajumbe wengine walioachia ngazi Yanga ni pamoja na Seif Ahmed, Mbaraka Igangula, Mzee Yusuf, Ally Mayay, Charles Mgondo  na Mohammed Bhinda.

KIM:SIKUTEUA WACHEZAJI STARS KWA UPENDELEO


KOCHA wa Taifa Stars Kim Poulsen amekana kupendelea katika uteuzi wa wachezaji wa kikosi hicho  na kusema kwamba alichagua wachezaji kutokana uwezo na sifa walizonazo na si kuangalia ni mchezaji wa timu gani.
Alisema nashangazwa na maalalamiko ya baadhi ya wadau wa soka ambao wamekuwa wakielekeza shutuma hizo ambazo hazina ukweli wowote. 
Baadhi ya wadau walimekuwa wakimlalamikia kocha huyo kutokana na kuchagua nyota wengi kwenye kikosi hicho wakitokea klabu ya Simba huku mahasimu wao Yanga, akiteua mchezaji mmoja tu.
Aliongeza kuwa kikosi chake ambacho kinajiandaa na mchezo wake wa kuwania kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast kitaenda bila ya nyota wake Nurdin Bakari na Thomas Ulimwenguni ambao walipata majeruhi wakati wa mazoezi yao na kusema kuwa watabaki wakijinoa kabla ya kuungana na wenzao watakaporudi ili kujiandaa.
Akizungumzia mchezo wao dhidi ya Ivory Coast utakaopigwa juni 2 huko Abdjan, Paulsen alisema  kikosi chake kinaiheshimu kutokana na kuwa na wachezaji nyota wengi wenye  uwezo kisoka kwa ambao wanacheza ligi za ulaya wakiwemo  Didier Dragba, Solomon Kalou, Yaya Toure, Kolo Toure na wengineo. 
Alisema pamoja na hilo hawaiogopi zaidi ya kuwataka wachezaji wa Stars kutambua hawana tofauti na Ivory Cost isipokuwa ni mbinu tu za hapa na pale ambazo anaamini kwa uwezo walichonacho wachezaji wa Stars wanaweza kushinda.na mechi yao dhidi ya Gambia.

Wachezaji wengine waliopo Stars ni pamoja na  makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar). Mabeki: Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba).
Viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba- U20), Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20).
Washambuliaji ni Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Ramadhan Singano (Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20),  Haruna Moshi (Simba) na John Bocco (Azam). 

CHIPUKIZI 10 WAPITA MCHUJO ASPIRE


Wachezaji 10 wamepita katika mchakato wa kusaka vipaji kwa chipukizi wenye umri chini ya miaka 14 kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream ambao uko chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliofanyika kuanzia Mei 21-26 mwaka huu. 
Watoto zaidi ya 1,500 walishiriki katika mchakato huo uliokuwa chini ya mng’amua vipaji (scout) Gisbert Xavier kutoka Hispania, na ulifanyika katika vituo vya Morogoro, Bagamoyo mkoani Pwani, na Kawe, Makongo, Magomeni, Tabata, Kitunda, Tandika, Ukonga na Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume kwa Dar es Salaam. 
Kituo cha Morogoro amechaguliwa Karim Hussein wa Shule ya Sekondari Nanenane, kituo cha Magomeni ni Joseph Mushi wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere wakati kituo cha Tabata ni Martin Tangazi. 
Tandika ni Ismail Ngakonda (Shule ya Sekondari Uwanja wa Ndege), Kitunda ni Nicholas Lauteri (Shule ya Sekondari Ulongoni), Omari Mbwai (Shule ya Sekondari Msongola) na Hamad Omari (Shule ya Sekondari Ulongoni). 
Kituo cha Ukonga ni James Msuva (Shule ya Sekondari Makongo) wakati Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ni Adolf Mtasigwa (Shule ya Sekondari Loyola) na Ally Hatibu (Shule ya Sekondari Kurasini). 
Mng’amuzi huyo wa vipaji anatarajia kufanya mchujo wa mwingine kabla ya chipukizi hao kwenda Nairobi, Kenya kwenye mchujo wa mwisho baada ya kambi ya ya siku nne kuanzia Juni 5-9 mwaka huu.


MENEJA TWANGA PEPETA AJIUNGA MASHUJAA MUSICA


 Mshauri wa Mashujaa Musica King Dodoo kulia akizungumza na waandishi wa habari wakati wakimtambulisha meneja mpya wa bendi hiyo Martine Sospeter (kati) kushoto ni Rais wa Mashujaa musica, Chaz Baba.

ALIYEKUWA meneja wa bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Martin Sospeter ametangaza kujiunga bendi ya Mashujaa Musica. 
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Martin alisema kwamba amejiunga Mashujaa Musica kwa ridhaa yake na wala si kwa lengo la kuidhoofisha au kuiua Twanga Pepeta, bali kuendeleza muziki wa dansi nchini. 
Alisema hana ugomvi na mkurugenzi wa Twanga Asha Baraka pamoja na kutangaza kuwa amemfukuza kazi wakati akiwa mkoani Mtwara na bendi yake  akimtuhumu kuihujumu bendi yake kitu ambacho hakina ukweli na  kimemuumiza sana kiasi cha kumtoa machozi.
 “juzi usiku nilishangazwa na kauli ya mkurugenzi wangu wa Asha Baraka ambaye namchukulia zaidi ya dada yangu akidai amenifukuza kazi kutokana kuhujumu bendi ikiwemo kushawishi wanamuziki kujiunga na bendi ya Mashujaa,  kauli ile ilinisikitisha sana kutokana na ukweli kwamba nilimuheshimu sana na kufanya naye kazi kwa  miaka 13 iweje hii leo aje anitolee maneno ya kunichafua katika vyombo vya habari,? 
“Sijawahi kuhusika na mpango wowote wa wasanii wa Twanga kuhamia Mashujaa na wala sikuwa nafahamu mpango huo zaidi ya kusikia fununu za chinichini na mwishowe wasanii hao kutangazwa kuhamia Mashujaa, hivyo napenda umma uelewe kwamba nimeondoka Twanga Pepeta na nimekabidhi kila kilichochao kama kuna kitu nadaiwa mtu alete uthibitisho,”alisema. 
Alisema ameshasaini mkataba wa kazi usio na mipaka, ambapo mbali na mkataba mnono, ameahidi kufanya kazi yake hiyo mpya kama ilivyokuwa Twanga ambapo alidumu nayo kwa muda mrefu na kuchangia kufika hadi hapo alipoachia, hivyo ameomba ushirikiano kwa uongozi, wanamuziki, Wadau na hata ninyi mwaandishi wa habari.

MCHAKATO WA KUMPATA MWAKILISHI MISS WORLD KUFUNGWA JUNI 4


WAREMBO wanaotaka kushindana katika shindano dogo la kumsaka mwakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Dunia (Miss World 2012) wameombwa kuendelea kuchukua fomu za kushindana katika kinyang’anyiro hicho na kuzirudisha kabla ya Juni 4. 
Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga amesema  kuwa wanatarajia kufanya mchujo wa washiriki Juni 5 kwa ajili ya kubakiza warembo 10 kwa ajili ya kuwania nafasi ya kushiriki katika mashindano ya Dunia yaliyopangwa kufanyika Agosti 18 kwenye ukumbi wa Dongsheng Fitness Center Stadium,  mjini Ordos, Inner Mongolia, China. 
Lundenga alisema kuwa  zoezi hilo lilisimamishwa kutokana na zuio la Serikali na  wakati huo, jumla ya warembo 12 walikuwa wamekwisha chukua fomu za kushiriki. Alisema kuwa muda wa kufanya mashindano hayo umekaribia na wanatarajia kuitangaza tarehe mpya hivi karibuni.

Alisema kuwa amefurahishwa na kasi ya kuchukua na kurejesha fomu, hata hivyo wanahitaji warembo wengi zaidi ili kuweza kupata wigo mpana kwa ajili ya kumsaka mrembo atakayewania taji la Dunia ambalo kwa sasa lina mikononi mwa mrembo kutoka Venezuela, Ivian Sarcos. 
“Tunakaribia kufanya mashindano madogo hivi karibuni, hivyo ni wajibu wetu kuwakumbusha warembo wanaotaka kuwania taji hilo kufanya hivyo kabla ya Juni 4 ili kuweza kuingia katika zoezi la mchujo,” alisema Lundenga. 
Alisema kuwa mpaka sasa jumla ya nchi 84 zimekwisha pata wawakilishi wao kwa ajili ya mashindano hayo. Nchi 32 pamoja na Tanzania bado hazija chagua wawakilishi wao katika mashindano hayo. 
 Fomu za kuomba kushiriki zinapatikana katika ofisi za Miss Tanzania za jijini na mawakala wote wa mashindano hayo katika mikoa ya Tanzania Bara.


MAKOCHA COPA COCA COLA KUSHIRIKI SEMINA YA FIFA


Makocha 35 wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kushiriki semina ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa ajili ya michuano ya vijana ya Copa Coca-Cola.
Semina hiyo itafanyika kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 4-9 mwaka huu chini ya mkufunzi kutoka FIFA, Ulric Mathiot. Makocha hao wanatakiwa kuripoti Juni 3 mwaka huu kwenye ofisi za TFF. 
Makocha hao na mikoa yao kwenye mabano ni Englihard Livigha (Mtwara), Joseph Sehaba (Dodoma), Ramadhan Ramadhan (Mjini Magharibi), Shaha Khamis Rashid (Kaskazini Unguja), Salum Ali Haji (Kusini Unguja), Mohamed Ali Khamis (Kaskazini Pemba), Mecky Maxime (Morogoro) na George Simon (Kagera). 
Haruni Dudu (Iringa), Maka Mwalwisi (Mbeya), Amos Mewa (Rukwa), Athuman Kilundumya (Tabora), Charles Mayaya (Shinyanga), Fulgence Novatus (Mwanza), James George (Mara), Amani Kongoro (Kigoma), Mtoro Likere (Ilala), Evarist Katomondo (Kinondoni), Shawal Bilanga (Temeke) na Rashid Chama (Arusha).

Wengine ni Francis Samatta (Ruvuma), Issac Gamba (Kilimanjaro), Aloyce Mayombo (Pwani), Jomo Puccey (Lindi), Justine Kanemela (Singida), Charles Msengi (Manyara), Mohamed Kampira (Tanga), Alfred Itael (Arusha), Nicholas Achimpota (Dodoma), Leonard Jima (Ruvuma), Leonard Malongo (Mwanza), Kesi Abdallah (Tanga), John Memba (Ilala) na Zuhura Kapama (Kigoma).

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


BASATA YAWATAKA WASANII KUONGEZA THAMANI KATIKA KAZI ZAO


 Mtendaji Mkuu wa asasi ya Musoma Handcrafts Haroun Sabili akitoa elimu kwa Wasanii na Wajasiriamali wa Sanaa za mikono kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa wiki hii.
 Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari wa BASATA Godfrey Lebejo akisisitiza jambo wakati akihitimisha programu ya Jukwaa la Sanaa wiki hii. Aliwataka wasanii kuongeza thamani katika kazi wanazozalisha.
 Akina mama Wasanii wa Sanaa za mikono wakiangalia moja ya kazi iliyobuniwa na kuongezewa uthamani. Kazi hiyo ilikuwa imetengenezwa na malighafi kutoka masalia ya viumbe wa baharini.
 Msanii akichunguza makini moja ya kazi ya Sanaa za mikono.
 Mama aking’aa na kazi ya Sanaa za Mikoni shingoni kwake.
Sehemu ya Wasanii na Wadau wa Sanaa za Mikono waliohudhuria kwenye programu ya Jukwaa la Sanaa wiki wakifuatilia darasa kwa makini.

Na Mwandishi Wetu
Huku kukiwa na juhudi za kutambuliwa na kuthaminiwa kazi za wasanii ndani na nje ya nchi, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii kuongeza thamani kwenye kazi zao ili kuzipa ubora zaidi.
Wito huo umetolewa mapema wiki hii na Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari wa BASATA Godfrey Lebejo wakati akihitimisha programu maalum iliyohusu Ubunifu, Utengenezaji na Uongezaji thamani katika Kazi za Sanaa kupitia Jukwaa la Sanaa.
Alisema kuwa, ubora katika Sanaa unapatikana pia kwa Wasanii kuangalia wenzao wanafanya nini na wao kupata ubunifu mpya kwa kuongeza vionjo, uthamani na ubunifu binafsi katika kuifanya kazi ya Sanaa kwanza kupendwa na baadaye kupewa thamani kubwa sokoni.
“Ni wazi Wasanii wetu wanapaswa kuzingatia uongezaji uthamani kwenye kazi wanazozifanya. Kubuni kazi ni suala moja lakini kuongeza uthamani katika kazi yako ili ivutie wengi na kuuzika kwa thamani kubwa ni suala lingine la kuzingatia” alisistiza Lebejo.
Aliongeza kuwa, kwa sasa kuna taarifa za Wakenya kununua kazi za Wasanii wetu kwa bei ya chini na baadaye kuziongezea ubunifu, thamani na kuziuza nje kwa bei  kubwa. Katika hili anasema, inatokana na wasanii wetu kutokuzingatia falsafa hiyo ya ubunifu na uongezaji thamani wa kazi zao.
“Tuna bahati ya kuwa na malighafi nyingi sana, baadhi zimeoneshwa hapa lakini suala hapa ni sisi kutumia ipasavyo malighafi hizo katika kubuni kazi zenye ubora na kuhakikisha tunazipa thamani stahiki tunapozisafirisha nje” alizidi kusisitiza.
Awali akiendesha darasa hilo maalum ambalo wiki hii lilikuwa mahsusi kwa ajili ya wasanii na wajasiriamali wa Sanaa za mikono (Handcrafts), Haroun Sabili kutoka asasi ya Musoma Handcraft alisema kuwa, Sanaa hizo zinahitaji ubunifu na umakini mkubwa kwani kinyume chake ni kutokuvutia na kupoteza uthamani.
Alitoa wito kwa Wasanii kujiunga katika vikundi na kuwa rasmi ili kuhakikisha kwanza,wanajenga mazingira ya kuwezeshwa lakini pia kupata mafunzo mbalimbali ambayo yatawafanya wazalishe kazi za Sanaa zenye ubora na thamani kubwa.
“Ni ngumu sana kuhudumia msanii mmoja-mmoja lakini mkiwa kwenye umoja ni rahisi sana kupata fursa za uwezeshaji hususan mafunzo katika kuongeza ubunifu na uthamani wa kazi zenu” alishauri Haroun.
Katika programu hiyo iliyohudhuriwa na wadau 72, elimu kuhusu ubunifu na uongezaji thamani kwenye kazi za Sanaa ilitolewa sambamba na malighafi mbalimbali na jinsi zinavyoweza kutumika kuzalisha kazi za mikono kuoneshwa.

AMOS MAKALLA AJITOA SIMBA SC

Mh.Makalla akitunuku nahodha wa Simba Juma Kaseja wakati wa sherehe za ubingwa wa Simba zilizofanyika Dar Live jumapili.


NAIBU Waziri wa habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Amos  Makalla amejitoa kattika kamati ya fedha ya klabu ya soka ya Simba.
Makalla  aliteuliwa na kamati ya utendaji ya Simba chini ya mwenyekiti wake Simba Ismail Aden Rage mwezi oktoba mwaka jana  sambamba na Geofrey Nyange 'Kaburu' ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo na makamu wake ni Adam Mgoyi, wajume wengine ni pamoja na  Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, katibu mkuu wa zamani wa Simba, Kassim Dewji na mdhamini wa zamani wa klabu hiyo Azim Dewji ni pamoja na Said Pamba,Juma Pinto, Abdul Mteketa na Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu.
Hata hivyo, Makala ambaye ni mbunge wa Mvomero alitangaza kujitoa nafasi hiyo kutokana na nafasi ya Unaibu Waziri na kusema kuwa analazimika kufanya hivyo ili kuweza kuvisaidia vilabu vya michezo yote nchini.

NURDIN, ULIMWENGU WAPELEKA AHUENI STARS

KIM Poulsen, kocha wa timu ya Taifa (Taifa Stars), amesema kupata nafuu na kurejea uwanjani kwa kiungo, Nurdin Bakari ni suluhisho la udhaifu katika safu ya kiungo ya timu hiyo. Bakari na mshambuliaji, Thomas Ulimwengu jana waliungana na wenzao katika mazoezi ya asubuhi kwenye Uwanja wa Karume ikiwa ni baada ya kuwa nje kwa zaidi ya wiki moja kutokana na kuwa majeruhi.

Ulimwengu alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya nyama za paja, wakati Bakari alikuwa majeruhi wa kifundo cha mguu.

Akizungumza mara baada ya mazoezi, Kim alisema endapo Bakari atapona haraka, basi atakuwa kwenye mpango wake wa kumtumia kwa ajili mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast baadaye mwezi ujao.

"Kama nilivyosema awali, kwa sasa nashughulikia kutafuta ufumbuzi wa matatizo niliyoona kwenye mechi dhidi ya Malawi kabla ya kuivaa Ivory Coast. Nachofurahi ni kurejea mazoezini kwa Bakari na Ulimwengu. Hawa ni wachezaji muhimu wanaweza kutusaidia kwenye mechi inayofuata. Bakari ni mzoefu mkubwa wa sehemu ya kiungo," alisema Kim.

Kim ambaye amekuwa akikosoa ubinafsi na kusisitiza umuhimu wa wachezaji wa kucheza kitimu, aliwakingia kifua chipukizi wake kwa kusema bado wanahitaji muda ili waweze kupata uzoefu.

"Uzoefu ni muhimu kwenye kazi yoyote ingawa hata yule asiyenao anatakiwa apewe fursa ili na yeye apate. Frank Domayo hakucheza vibaya siku ila alikosa uzoefu, Nurdin Bakari ni mzoefu anaweza kusaidia." Kim.

Aidha, Kim amewataka wachezaji wake kutohofia majina makubwa ya wachezaji wa Ivory Coast siku watakapopambana nao ugenini mjini Abidjan.

Ivory Coast ina wachezaji wenye majina makubwa kama Didier Drogba, Yahya Toure, Kolo Toure and Solomon Kalou wanaocheza soka Ligi Kuu England.

Alisema ana imani wachezaji wake wana sifa ya kimataifa na amewataka kutokuwa na hofu ya majina, bali wacheze kwa kushambulia kwa vile ni muhimu kupata bao ugenini.

CHANZO:GAZETI LA MWANANCHI

Monday, May 28, 2012

SHULE ZITAKAZOSHIRIKI MICHUANO YA AIRTLE RISING STARS ZAKABIDHIWA VIFAA



Dar es Salaam, Jumatatu Mei 28, 2012…Airtel Tanzania leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu za shule za sekondari 24 zitakazoshiriki kwenye michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 maarufu kama Airtel Rising Stars ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumatano, Mei 30, ngazi ya Mkoa.
Shule zitakazoshiriki kwenye michuano hiyo ni zile zilizofanya vyema kwenye michuano ya shule za sekondari (UMISSETA), ambazo ni Lindi sekondari, Mpunyule na Nkowe zote za Mkoa wa Lindi, Southern Highland, Mbeya Day na Wenda Sekondari kutoka Mbeya.
Nyingine ni Mbande Sekondari, Kurasini na Kiravi (Temeke), Airwing, Benjamini Mkapa na Msogola Sekondari (Ilala), Twiga Sekondari, Goba na Makongo Sekondari (Kinondoni), Sinoni, Kaloleni na Bishop Durning (Arusha).
Timu hizo zote zimethibitisha ushiriki wao na kuahidi kufanya vizuri ili kushinda mechi zao. Mechi za mikoa zitatumika kuchangua timu kombaini zitakazowakilisha mikoa kwenye mashindano ya Airtel Rising Stars ngazi ya taifa yatakayoanza Juni 9 mpaka Juni 17 Jijini Dar es Salaam.
Katika hatua nyingine, Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) leo imetoa ratiba ya michuano ya ARS ngazi ya mkoa kwa timu 24. Ratiba hiyo inaonyesha kuwa shule ya …….itacheza na ……….kwenye ufunguzi wa Kinondoni, ………….na…………..kutoka Ilala zitapambana kwenye mechi ya ufunguzi. …………. Itacheza na …………kutoka Temeke huku………..ikicheza na ………….kutoka Arusha.
Kutoka Mbeya, mechi ya ufunguzi itakuwa baina ya ………….na ……………….kwenye uwanja wa…………Mkoa wa Lindi shule ya ……….itacheza na ……………..kwenye ufunguzi huo.
Wakati timu za wavulana zikatarajiwa kushindana kwenye ngazi ya mkoa ili kuchanguliwa kucheza michuano ya Taifa, timu moja kutoka kila Mkoa itafuzu moja kwa moja na kufanya timu zitakazoshiriki ngazi ya taifa kuwa 12, sita za wavulana na sita wasichana.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, Meneja Masoko na Matangazo Airtel Tanzania Rahma Mwapachu alisema Airtel inajivunia ushirika wake na moja ya Klabu kubwa duniani – Machester United, kuinua kiwango cha mpira wa miguu nchini Tanzania na Afrika.
 ‘Tunaamini ya kuwa kwa ushirikiano wetu na Manchester United na TFF tutakuza kwa kiasi kikubwa kiwango cha mpira wa miguu hapa nchini Tanzania. Tunaamini vijana wakiandaliwa vizuri wanaweza’.
Mwapachu alishukuru Wizara ya Habari, Vijana, Utamanduni na Michezo kwa ushirikiano wanaotoa ili kukuza mpira hapa nchini.
Airtel Rising Stars ni mpango kabambe wa Afrika nzima ambao ni kuibua na kukuza vipaji vya wanasoka wanaochipukia, wavulana na wasichana wenye umri wa miaka chini ya kumi na saba ambao watapata muda muafaka wa kuonyesha vipaji vyao na kukutana na waatalum wa mpira wa miguu na kupata mafunzo zaidi hivyo kukuza vipaji vyao.
Mwaka jana, Klabu ya Manchester United ilitoa walimu wake wa soka la vijana kufundisha kliniki za soka za kimataifa zilizofanyika Tanzania, Afrika Kusini na Gabon ambapo walishiriki walipata nafasi ya kufundisha jinsi ya kucheza mpira wa miguu kwa mtindo wa Manchester United.
Kliniki ya aina hiyo itafanyika Jijini Nairobi Agosti mwaka huu kwa nchi zinazozungumza Kingereza Tanzania ikiwemo. Nairobi pia itakuwa mwenyeji wa mashindano ya Airtel Rising Stars inter-continental ambayo itashirikisha nchi 14 ambapo Airtel inafanya biashara. Tanzania itawakilishwa na mshindi wa fainali za taifa pamoja na wachezaji sita bora, watatu wavulana na watatu wasichana.

KIM POULSEN:MAMBO MAZURI HAYATAKI HARAKA

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen amesema timu yake inaweza kufanya vizuri, lakini lazima wapewe muda.
Gazeti la Habari Leo, limeandika leo kwamba kutokana na hali hiyo amewaomba mashabiki nchini kuwa wavumilivu na kwamba ipo siku wataikubali na kuanza kuwashangilia wachezaji.
“Ni mwanzo mzuri wa safari yangu, kutoka sare nadhani ni mwanzo mzuri, sio matokeo mabaya kwangu na wala sio matokeo mabaya kwa Malawi, nahitaji kupewa muda zaidi,”alisem Kim baada ya mchezo wa kirafiki kati ya Stars na Malawi juzi uliomalizika kwa timu hizo kutofungana.
Alisema amefurahishwa na kiwango ambacho timu yake ilikionesha na kuomba kupewa
muda zaidi ili ifanye vizuri kwani kikosi chake bado ni kichanga na kinaundwa na wachezaji wengi chipukizi hivyo hawezi kuibadilisha timu hiyo kipindi cha wiki moja tokea aanze kuifundisha timu hiyo.
Kocha huyo aliyekuwa akifundisha timu za taifa za vijana aliwataka wachezaji wa timu hiyo
kucheza vizuri muda wote ili kuwanyamazisha mashabiki wachache waliokuwa wakiizomea
kwenye mchezo huo.
“Ukiona mashabiki wanazomea ujue bado haujawafurahisha, nafikiri wakicheza vizuri hawatazomewa, naelewa hisia za mashabiki kuwa wanataka timu ishinde na ichezea vizuri lakini hilo lisipotokea ni wazi watazomea,”alisema Kim.
Taifa Stars itacheza na timu ya Taifa ya Ivory Coast Juni 2 huko Abdijani kujiandaa na mchezo wa awali wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia.
Mbali na miamba hiyo ya soka ya Afrika Magharibi Stars iko kundi moja na Gambia na
Morocco. 

SUMA LEE KUITAMBULISHA UTANIKUMBUSHA CLUB BILICANAS J'2 HII


Sunday, May 27, 2012

TWIGA STARS YALALA 2-1

Twiga Stars

TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Twiga Stars, imeanza ‘vibaya kidodo’ kampeni za kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa kwa wanawake, baada ya kufungwa mabao 2-1 jioni hii mjini Addis Ababa na wenyeji, Ethiopia.
Twiga sasa inahitaji ushindi wa 1-0, Juni 16, katika mchezo wa marudiano mjini Dar es Salaam, ili kukata tiketi ya kucheza fainali hizo kwa mara ya pili mfululizo, Novemba mwaka huu, Equatorial Guinea, zikiwa ni za nane katika historia ya michuano hiyo

TFF YAAGIZA YANGA KUFANYA UCHAGUZI JULAI 15

MASHINDANO YA JUDO YARINDIMA JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa Judo Tanzania Bw, Khalifa Kiumbemoto katikati akifuatila kwa makini Mashindano ya Mchezo huo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Landmark jijini Dar es Salaam wa kwanza kushoto kwake ni Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Habari na Michezo Bw. Charles Mattoke na wapili kushoto kwake ni Mdhamini wa Mashindano hayo kutoka Germin Copperation LTD Bw. Yulliy Tarverdyan. Katika Mashindano hayo Watanzania walionekana kushindwa na wachezaji kutoka Zanzibar.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Mchezaji wa Judo kutoka CCP Polisi Moshi (wa juu) Bw. Kisamerwa Magangwa akiwa amemgeuza mshindani wake Bw,.Mohammed Juma kutoka Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam katika mchezo huo.
Baadhi ya mashabiki walioudhuria katika
mpambano wa mchezo huo wakifuatilia kwa makini.
Wataalamu wa kufuatilia muda katika mashindano ya mchezo huo wakifuatilia kwa umakini mchezo huo.

BEYONCE MVUTO PALEPALE, AFANYA ONYESHO LAKE LA KWANZA TANGU AITWE MAMA

NYOTA wa muziki nchini Marekani Beyonce juzi amefanya onyesho lake la kmwanza tangu ajifungue mtoto wake wa kwanza, Blue Ivy mwezi januari 2012.
Katika onyesho hilo, lililofanyika ukumbi wa  Revel resort katika jiji la Atlantic City, alionekana mwenye kupendeza zaidi huku akinakshiwa na kivazi chake matata kilichomkaa vema kwenye mwili wake wenye mvuto wa kike.
Kama hiyo haitoshi, nyota huyo mke wa Rapa Jay Z, aliweza kumudu ipasacyo jukwaa huku akitumbuiza kwa nyimbo zake kadhaa zikiwemo
"Run the World (Girls)," "Single Ladies," "Countdown",  "Halo, na nyinginezo.

BONDIA IDDY MNYEKE AJINOA KUMKABILI FADHIRI AWADHI JUNE 9

Bondia Iddy Mnyeke kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Vitor Njait wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya ngumi ya Ilala Mnyeke anajitahalisha na mpambano wake dhidi ya Fadhiri Awadhi utakaofanyika June 9 katika ukumbi wa Frensi kona Manzese Dar es salaam .
Bondia Iddy Mnyeke kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Vitor Njait wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya ngumi ya Ilala Mnyeke anajitahalisha na mpambano wake dhidi ya Fadhiri Awadhi utakaofanyika June 9 katika ukumbi wa Frensi kona Manzese Dar es salaam .Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com



TFF YAWAPIGA CHINI WAZEE YANGA, KATIBU MKUU APEWA MAJUKUMU

Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana Mei 26 mwaka huu ili kutoa mwongozo wa nini kifanyike ndani ya Yanga baada ya wajumbe wake kudhaa kujiuzulu.
Kamati ya Uchaguzi ya Yanga ilikuwa imeomba mwongozo huo TFF.
Baada ya kupata taarifa rasmi kutoka Yanga, Kamati imebaini kuwa Kamati ya Utendaji ya Yanga imekosa akidi baada ya wajumbe wake wengi kujiuzulu hivyo kutokuwa na uwezo wa kufanya uamuzi kwa mujibu wa Ibara ya 32(1) ya Katiba ya klabu hiyo.
Hivyo, Kamati imetoa mwongozo kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF ambayo ndiyo msimamizi wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga kuwa ili Kamati ya Utendaji ya Yanga iwe na nguvu za kikatiba kufanya shughuli zake ikiwemo uamuzi wa masuala mbalimbali ndani ya klabu hiyo ni lazima iwe na akidi.
Kwa mujibu wa Ibara ya 29(3) ya Katiba ya Yanga nafasi zilizo wazi katika Kamati ya Utendaji zinatakiwa kujazwa katika Mkutano Mkuu wa Kawaida ujao.
Pia Kamati imebaini uteuzi wa kujaza nafasi zilizo wazi za wajumbe uliofanywa na Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mei 21 mwaka huu ni batili kwa vile Kamati ya Utendaji iliyofanya uteuzi huo haikuwa na akidi.
Ili kupata akidi na kufanya uamuzi Kamati ya Utendaji ya Yanga yenye wajumbe 13 inatakiwa kuwa na asilimia 50 ya wajumbe wote, hivyo ili wafanye uamuzi halali hawatakiwi kupungua saba.
Kwa wajumbe ambao hawajajiuzulu; Sarah Ramadhan, Mohamed Bhinda, Tito Osoro na Salim Rupia kwa sasa hawawezi kufanya shughuli zozote za Yanga hadi nafasi zilizo wazi katika Kamati ya Utendaji zitakapojazwa.
Kama inavyoelekeza Katiba ya Yanga, shughuli za kila siku za klabu hiyo zitaendelea kufanywa na Sekretarieti ya Yanga ambayo kiongozi wake ni Katibu Mkuu.
Alex Mgongolwa
Mwenyekiti
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji

MABINGWA WA SOKA TZ SIMBA SC WAKIJIVINJARI MITAA YA JIJI LA DSM








MISS SINZA KUANZA KUJINOA JUNI MOSI

Na Mwandishi Wetu
MAZOEZI ya warembo wataowania taji la Miss Sinza 2012 yamepangwa kuanza Juni Mosi kwenye ukumbi wa Ten Star Lounge (Mawela Social Hall) ulipo karibu na hotel ya Vatican City uliopo Sinza.
Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary(pichani) alisema kuwa mazoezi hayo yataanza saa 10.00 jioni na ni ya wazi kwa warembo wenye nia ya kutaka kuwania taji na zawadi nono za washindi wa mwaka huu ambao wataiwakilisha Sinza kwenye mashindano ya Kanda ya Kinondoni, Miss Tanzania na baadaye katika mashindano ya Dunia “Miss World”.
Majuto alisema kuwa fomu za washiriki zitatolewa hapo hapo kwenye ukumbi wa mazoezi na wengine wanaotaka kushiriki katika mashindano hayo wanatakiwa kufika ofisi za Mama Tike Hair Fashion and Boutique zilizopo Sinza Kumekucha kituoni, Ofisi za Miss Tanzania (Posta),  ofisi za SMP zilizopo Kinondoni Mkwajuni, Brake Point (Kijitonyama na Posta) na kupitia mtandao wa balilemajuto.blogspot.com, sufiani mafoto.blogspot.com.
Alisema kuwa kamati ya Miss Sinza kwa sasa ipo katika mikakati mbali mbali ya kusaka wadhamini kwa ajili ya kufanikisha mashindano hayo yanayotarajiwa kuwa bora kabisa mwaka huu.
“Tunaomba wadhamini ikiwa ni makampuni, wafanya biashara, wadau wa masuala ya urembo ambao wanataka kujitangaza kupitia mashindano haya kujitokeza kusaidia waandaaji kwani lengo kubwa ni kuona Sinza inafanya mashindano bora na yenye kuleta mafanikio makubwa kwa kutwaa taji la Miss Tanzania na lile la Dunia,” alisema Majuto.
Alifafanua kuwa  wameandaa mikakati na mipango mbali mbali ili kuhakikisha Sinza mwaka huu inapata mafanikio makubwa katika mashindano ya Miss Tanzania na yale ya Dunia.

MECHI YA STARS, MALAWI YAINGIZA MIL.40



Mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Malawi (The Flames) iliyochezwa Mei 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 40,980,000.

Mapato hayo yametokana na washabiki 10,767 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 51,000 na sh. 20,000. Washabiki 9,365 walikata tiketi za sh. 3,000.

Asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 6,251,186 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 4,999,800), waamuzi (sh. 1,105,000), usafi na ulinzi (sh. 2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing Construction (sh. 2,000,000) na umeme (sh. 300,000).

Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 4,714,803, asilimia 10 ya uwanja sh. 2,357,401, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 1,178,701, asilimia 20 ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 4,714,803 na asilimia 45 ya TFF (sh. 10,608,306).