Ronaldo alifunga bao kwa kichwa dakika ya sita ambalo
lilikuwa la 35 anaifungia Real Madrid kwenye mashindano yote msimu huu. Santander ilicheza pungufu baada ya Domingo Cisma kutolewa
nje kwa kadi nyekundu dakika ya 39 kwa kuushika mpira kwa makusudi mara ya pili. Karim Benzema akapiga mabao dakika ya 45 na 89, katikati ya
bao la Angel di Maria, aliyecheza mechi ya kwanza tangu Desemba 17. Barcelona leo wanaikaribisha Valencia inayoshika
nafasi ya tatu.
Sunday, February 19, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



0 Maoni::
Post a Comment